Monday, 30 January 2017

Mkuu wa Wilaya ya Nzega Mheshimiwa Godfrey Ngupula akitoa maelezo ya kuondoa hofu  kwa wananchi juu ya imani potofu za upasuaji wa wagonjwa katika majengo mapya ya upasuaji kwenye vituo vya Afya.
Hofu hiyo ilisababishwa na imani potofu zilizojengwa na kuenea sana miongoni mwa wananchi katika Kata ya Itobo na kuwasababishia woga kutibiwa katika jengo hilo jipya la upasuaji Itobo.

Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali ya wilaya ya Nzega Dr. Edward Sengo akisoma taarifa fupi ya jengo la upasuaji kituo cha afya Itobo .

Mheshimiwa Naibu Waziri wa Afya Dr.Hamis A. Kigwangalla akisalimiana na wananchi kituo cha afya Lusu mara baada ya kuwasili 14 Desemba,2016.
Pembeni yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Nzega ndugu James Jacob Mtalitinya akionesha furaha yake.

Friday, 27 January 2017

MATUKIO MBALIMBALI


NZEGA NI WILAYA KATIKA MKOA WA TABORA. 

Mheshimiwa Naibu Waziri wa Afya wa kwanza kulia pamoja na mkuu wa wilaya na makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Nzega wakisikiliza taarifa fupi ya mradi wa jengo la upasuaji katika kituo cha afya Itobo siku ya uzinduzi wa jengo hilo tarehe 14 Desemba,2016.

MAPOKEZI YA MWENGE NZEGA DC

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Nzega  ndugu J.J.Mtalitinya akionesha furaha kuwa sasa atapokea na kukimbiza Mwenge ...