Tuesday, 18 July 2017

MAPOKEZI YA MWENGE NZEGA DC


Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Nzega  ndugu J.J.Mtalitinya akionesha furaha kuwa sasa atapokea na kukimbiza Mwenge katika Halmashauri yake tarehe 16.07.2017 Jumapili.
Hapa ni SIGILI Kata ya Sigili akisubiri mwenge pamoja na viongozi wengine wa mkoa.


Makamanda na viongozi wa Jeshi nao hawakuwa mbali katika kusubiri kupokea Mwenge wa Uhuru.Hapa viongozi hawa wanaonekana wakisalimiana .




Mkuu wa mkoa Tabora(mwenye kofia) hakuwa mbali na mapokezi hayo...
alishiriki kikamilifu katika maandalizi ya kupokea Mwenge wa uhuru ,hapa anateta kitu na moja ya viongozi katika mkoa wetu wa Tabora.

unaweza kuona jinsi gani sherehe za maandalizi ya kupokea mwenge zilivyokuwa na furaha katika siku hiyo. Mkuu wa wilaya ya Urambo akionekana kuwa na furaha kubwa na kuonesha kwamba bado anao uwezo wa kucheza mziki wa Ki-Afrika.



hayawi hayawi hatimaye ulifika wakati ambapo viongozi wa mbio za mwenge walifika na kupokelewa na skauti kwa kuvalishwa skafu na kuonesha kwamba sasa shughuli za uangalizi siyo shinyanga bali katika mkoa wa Tabora. kweli ni furaha na amani kupokea viongozi hawa na kushiriana nao katika kukagua miradi mbalimbali katika wilaya ya Nzega.
 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akimkabidhi Mwenge Mkuu wa Mkoa wa Tabora.
 Hapa mkuu wa mkoa wa Tabora akishikana mkono na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,hii ikionesha kupongezana kwa kwa zoezi walilolifanya katika siku hii. kwamba hongera ndugu kwa kukamilisha mbio za mwenge mkoani kwako na karibu Mwenge Mkoani kwangu .
 hapa kiongozi wa mbio za mwenge akionesha ukakamavu katika kujiandaa kutembea na mwenge kuwapelekea viongozi wa kiserikali katika mkoa wa Tabora.
 ilifika wakati ambapo viongozi wa serikali na majeshi walikamilisha furaha yao ya kuupokea mikononi mwao Mwenge wa uhuru.
 Mkuu wa mkoa wa Tabora akisoma risala.
 Mkuu wa mkoa wa Tabora akimkabidhi mkuu wa wilaya ya Nzega Mwenge wa Uhuru tayari kuukimbiza katika halmashauri ya wilaya ya Nzega.

 viongozi wa kisiasa na serikali walishirikiana kuupokea Mwenge wa Uhuru,Mheshimiwa  Selemani J. Zedi Mbunge wa jimbo la Bukene akionesha furaha yake kuupokea mwenge.
 katika kijiji hiki cha Sigili ndipo mwenge ulipokelewa lakini pia ndipo mahali pa kwanza kufunguliwa kwa mradi wa madarasa mawili kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha tano na sita.

mara baada ya ufunguzi huo kiongozi wa mbio za mwenge alihutubia wananchi akiwasisitiza katika kilimo cha tumbaku na urinaji wa asali kwani mkoa wa Tabora ni moja ya mikoa inayotoa asali kwa wingi.

Wednesday, 5 April 2017

WATOTO WENYE ULEMAVU WA NGOZI, TATU NA MASUNGA WAPELEKWA KITUO CHA WATOTO - URAMBO

hapa ndipo MWASAMBO.








Mheshimiwa Diwani kata ya WELA P.Makonda picha ya pamoja na watoto wenye ulemavu








babu wa watoto Tatu na Masunga





Familia ya watoto wenye ulemavu wa ngozi huko Mwasambo kata ya Wela.





Watoto kwenye picha ya pamoja na wenzao kituo cha watoto huko URAMBO.

Watoto kwenye picha ya pamoja na wenzao kituo cha watoto huko URAMBO.

Watoto kwenye picha ya pamoja na wenzao kituo cha watoto huko URAMBO.











Tuesday, 4 April 2017

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Nzega Mh.Michael Bundala akiwa katika ziara kikazi katika kata ya ITOBO akikagua jengo la soko.

Monday, 30 January 2017

Mkuu wa Wilaya ya Nzega Mheshimiwa Godfrey Ngupula akitoa maelezo ya kuondoa hofu  kwa wananchi juu ya imani potofu za upasuaji wa wagonjwa katika majengo mapya ya upasuaji kwenye vituo vya Afya.
Hofu hiyo ilisababishwa na imani potofu zilizojengwa na kuenea sana miongoni mwa wananchi katika Kata ya Itobo na kuwasababishia woga kutibiwa katika jengo hilo jipya la upasuaji Itobo.

Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali ya wilaya ya Nzega Dr. Edward Sengo akisoma taarifa fupi ya jengo la upasuaji kituo cha afya Itobo .

Mheshimiwa Naibu Waziri wa Afya Dr.Hamis A. Kigwangalla akisalimiana na wananchi kituo cha afya Lusu mara baada ya kuwasili 14 Desemba,2016.
Pembeni yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Nzega ndugu James Jacob Mtalitinya akionesha furaha yake.

Friday, 27 January 2017

MATUKIO MBALIMBALI


NZEGA NI WILAYA KATIKA MKOA WA TABORA. 

Mheshimiwa Naibu Waziri wa Afya wa kwanza kulia pamoja na mkuu wa wilaya na makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Nzega wakisikiliza taarifa fupi ya mradi wa jengo la upasuaji katika kituo cha afya Itobo siku ya uzinduzi wa jengo hilo tarehe 14 Desemba,2016.

MAPOKEZI YA MWENGE NZEGA DC

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Nzega  ndugu J.J.Mtalitinya akionesha furaha kuwa sasa atapokea na kukimbiza Mwenge ...