Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Nzega ndugu J.J.Mtalitinya akionesha furaha kuwa sasa atapokea na kukimbiza Mwenge katika Halmashauri yake tarehe 16.07.2017 Jumapili.
Hapa ni SIGILI Kata ya Sigili akisubiri mwenge pamoja na viongozi wengine wa mkoa.
Makamanda na viongozi wa Jeshi nao hawakuwa mbali katika kusubiri kupokea Mwenge wa Uhuru.Hapa viongozi hawa wanaonekana wakisalimiana .
Mkuu wa mkoa Tabora(mwenye kofia) hakuwa mbali na mapokezi hayo...
alishiriki kikamilifu katika maandalizi ya kupokea Mwenge wa uhuru ,hapa anateta kitu na moja ya viongozi katika mkoa wetu wa Tabora.
unaweza kuona jinsi gani sherehe za maandalizi ya kupokea mwenge zilivyokuwa na furaha katika siku hiyo. Mkuu wa wilaya ya Urambo akionekana kuwa na furaha kubwa na kuonesha kwamba bado anao uwezo wa kucheza mziki wa Ki-Afrika.
hayawi hayawi hatimaye ulifika wakati ambapo viongozi wa mbio za mwenge walifika na kupokelewa na skauti kwa kuvalishwa skafu na kuonesha kwamba sasa shughuli za uangalizi siyo shinyanga bali katika mkoa wa Tabora. kweli ni furaha na amani kupokea viongozi hawa na kushiriana nao katika kukagua miradi mbalimbali katika wilaya ya Nzega.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akimkabidhi Mwenge Mkuu wa Mkoa wa Tabora.
Hapa mkuu wa mkoa wa Tabora akishikana mkono na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,hii ikionesha kupongezana kwa kwa zoezi walilolifanya katika siku hii. kwamba hongera ndugu kwa kukamilisha mbio za mwenge mkoani kwako na karibu Mwenge Mkoani kwangu .
hapa kiongozi wa mbio za mwenge akionesha ukakamavu katika kujiandaa kutembea na mwenge kuwapelekea viongozi wa kiserikali katika mkoa wa Tabora.
ilifika wakati ambapo viongozi wa serikali na majeshi walikamilisha furaha yao ya kuupokea mikononi mwao Mwenge wa uhuru.
Mkuu wa mkoa wa Tabora akisoma risala.
Mkuu wa mkoa wa Tabora akimkabidhi mkuu wa wilaya ya Nzega Mwenge wa Uhuru tayari kuukimbiza katika halmashauri ya wilaya ya Nzega.
viongozi wa kisiasa na serikali walishirikiana kuupokea Mwenge wa Uhuru,Mheshimiwa Selemani J. Zedi Mbunge wa jimbo la Bukene akionesha furaha yake kuupokea mwenge.
katika kijiji hiki cha Sigili ndipo mwenge ulipokelewa lakini pia ndipo mahali pa kwanza kufunguliwa kwa mradi wa madarasa mawili kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha tano na sita.
mara baada ya ufunguzi huo kiongozi wa mbio za mwenge alihutubia wananchi akiwasisitiza katika kilimo cha tumbaku na urinaji wa asali kwani mkoa wa Tabora ni moja ya mikoa inayotoa asali kwa wingi.